September 6, 2014


Akitokea kwenye benchi Paul Modo Kiongera amepiga bao mbili na kuipa Simba ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao moja la Simba lilifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Singano alifunga bao hilo baada ya Okwi kupiga shuti kali lililotemwa na kipa naye akakuta ‘dodo’ uani, na kujilia atakavyo.
Lakini Kiongera pia alifunga bao la kwanza baada ya kupokea krosi safi ya Okwi aliyekuwa amemtoka beki wa Gor.
Gor ambao ni wakongwe na mabingwa mara nyingi zaidi wa Kenya, walitawala kipindi cha kwanza na kuwanyima raha mashabiki wa Simba.

Lakini kipindi cha pili mambo yakageuka na wao kuonekana hawana cha kufanya dhidi ya vijana wa Patrick Phiri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic