Kuondoka
kwa Ángel di María aliyejiunga na manchester United kumeiwekea Real Madrid
rekodi mpya.
Kwamba
ina kikosi bila ya kuwa na mchezaji hata mmoja kutoka nchini Argentina.
Haijawahi
kutokea toka mwaka 2006, imekuwa ni lazima iwe na mchezaji kutoka Argentina.
Kihistoria
imekuwa na wachezaji imara kutoka katika nchi hiyo, angalia kama Ángel di
María, Fernando Gago, Ezequiel Garay na Gonzalo Higuaín.
Tokea
mwaka 1911, ilikuwa na wachezaji nyota zaidi kutoka Argentina, mfano ndugu
Sotero na José Eulogio ambao wametajwa kuwa kati ya wachezaji nyota zaidi 100
wa Madrid.
Usisahau
anayeaminika kuwa mchezaji bora zaidi ya Madrid, Alfredo di Stéfano, anatokea
Argentina.
Madrid
inaaminika imekuwa moja ya timu yenye wachezaji wenye mafanikio kutoka
Argentina, lakini msimu huu kikosi hicho kitakwenda bila ya Muargentina hata
mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment