Baada
ya Diego Simeone kusimishwa kwenye mechi ya watani wa Hispania, Real Madrid na
Atletico Madrid, sasa jukumu hilo amekabidhiwa Germán Burgos ‘Mono’.
Inaaminika
Mono ndiye mtu wa Atletico Madrid asiyeopenda Madrid kuliko wote.
Madrid
ilimsumbua sana wakati akiwa kipa wa A Atlético na sasa ataiongoza pale Santiago
Bernabéu, keshokutwa Jumamosi.
Siku
zote Mono amekuwa akiizungumzia mechi aliyokuwa langoni na Madrid ikashinda
mabao 2-1 yote yakifungwa na Luis Figo.
Hata
hivyo alijitahidi kuokoa mkwaju wa penalti ambao ulimuumiza pua na damu kuvuja
kwa wingi.
Hakuwa
kushinda dhidi ya Madrid hadi alipokuwa kocha msaidizi.
Wakati
fulani aliwahi kumuambia Kocha Jose Mourinho akiwa Madrid: “Mimi siyo
Villanova, ntakuvunja shingo yako.”
Hata
hivyo katika mechi iliyofuata, Atletico ikanagukia pua kwa Madrid. Swali je,
kesho akiwa bosi kwa muda atalipa kisasi?
0 COMMENTS:
Post a Comment