Na Saleh Ally
DIRISHA la uhamisho kwenye
Ligi Kuu England limefungwa usiku wa kuamkia jana huku kukiwa na gumzo kubwa la
usajili.
Kati ya usajili uliowavutia
wengi uliomalizia dirisha hilo ni ule wa Ramadel Falcao ambaye ametua
Manchester United kwa mkopo akitokea AS Monaco ya Ufaransa pamoja na Danny Welbeck
kutoka Man United na kujiunga na Arsenal kwa pauni milioni 16.
Mambo yamebadilika kidogo,
kama ilivyo hapa nyumbani mara nyingi usajili mkubwa ni Yanga, Simba na Azam FC
tu, safari hii karibu kila timu England imefanya usajili na kutumia fedha
nyingi, hali ambayo imeshangaza na kuonyesha ushindani kwenye ligi hiyo utakuwa
juu zaidi.
Katika fedha za usajili,
upande wa manunuzi kwa klabu zote 20 za Premiership, pauni milioni 857.7
zimetumika au euro bilioni 1.09 (zaidi ya Sh trilioni 2.3).
Hiyo ni rekodi mpya kwa
kuwa msimu uliopita, pauni milioni 760 na ushee ndizo zilitumika, lakini safari
hii tena katika siku mbili za mwisho, imezidi hadi kufikia pauni milioni 850.
Manchester United pekee imetumia
pauni milioni 153.1 na kuwa klabu iliyotumia fedha nyingi zaidi katika
manunuzi. Huku ikiwa imeuza wachezaji kwa pauni milioni 31.2, maana yake sahihi
hasa iliyotumia ni pauni milioni £122.
Timu ambayo imetumia kidogo
zaidi ni Stoke City ambayo imetoa pauni milioni 3.4 tu katika usajili ili
kupata wachezaji wapya. Pia ikauza kwa fedha chache zaidi kuliko klabu nyingi
19 ambayo ni pauni milioni 3.
Katika klabu hizo 20,
zilizoingiza faida ni tatu tu ambazo ni Southampton, Tottehham na Chelsea.
Southampton imeongoza kwa
kuingiza faida baada ya kuwauza ghali wachezaji wake watatu ambao ni Adam
Lallana, Luke Shaw na Rickie Lambert.
Inayoshangaza zaidi ni
Chelsea, ilionekana imetoa zaidi na kuwa moja ya timu imara zaidi katika msimu
huu katika mechi za mwanzo lakini bado imeingiza faida.
Faida:
Timu zilizopata faida ni
tatu tu ambazo ni Southampton ambayo imeingiza faida ya pauni milioni 30.7
baada ya kuwa imefanya biashara ya kuuza wachezaji kwa jumla ya pauni milioni
88.5 na kununua kwa pauni 57.9 tu.
Tottenham inafuatia kwa
kuwa imeuza wachezaji kwa pauni milioni 40.7 na kununua kwa pauni milioni 34.2
tu, hivyo kufanikiwa kuingiza faida ya pauni milioni 6.5.
Chelsea ndiyo timu ya tatu
na ya mwisho katika kuingiza faida katika Premier League kwa kuwa ilinunua
wachezaji kwa pauni milioni 87.7 na kuuza kwa pauni milioni 88.5. hivyo faida
yake ni pauni 800,000 ambazo zinaingia kibindoni.
Timu nyingine 17
zilizobaki, hakuna hata moja iliyofanikiwa kuingiza faida kwenye Premier
League. Maana yake zote zimetoboka mifuko kuhakikisha zinajiimarisha zikihofia
msimu huu kuwa utakuwa mgumu maradufu ukilinganisha na uliopita.
TIMU 10 ZILIZOONGOZA KUTOA FEDHA KWA
AJILI YA USAJILI (*FEDHA HIZO NI KWA PAUNI MILIONI)
KLABU
IMETOA
IMEINGIZA IMETUMIA/PATO
GHALI ZAIDI
Man United £153.1
£31.2
£122
Angel Di Maria (£59.7)
Liverpool £116.8
£81.1
£35.7
Adam Lallana (£25.0)
Chelsea £87.7
£88.5
£0.8
Diego
Costa (£32.0)
Arsenal
£78.2
£31.8
£46.4
Alexis Sanchez (£35.0)
Southampton
£57.9
£88.6
£30.7
Shane Long (£12.0)
Man City
£54.5
£22.5
£32.0 Eliaquim Mangala (£32.0)
Hull City
£39.4
£15.0
£24.4
Abel Harnandez (£10.0)
Newcastle
£37.8 £12.9
£24.9 Remmy Cabella (£12.0)
QPR
£36.5
£15.5
£21.0 Sandro (£10.0)
West Ham
£34.5 £3.5
£31.0 Enner Valencia (£12.0)
Fedha
zilizotumika kwa usajili kwa kila msimu tokea 2004:
2004-05 £265 milioni
2005-06 £305
milioni
2006-07 £320
milioni
2007-08 £645
milioni
2008-09 £670
milioni
2009-10 £480
milioni
2010-11 £590
milioni
2011-12 £545
milioni
2012-13 £610
milioni
2013-14 £760
milioni
2014-15 £835
milioni
0 COMMENTS:
Post a Comment