NDUMBARO AKIWA MAKAO MAKUU YA FIFA, ZURICH USWISS. |
Mwanasheria mahiri nchini, Dk Damas Daniel Ndumbaro, kwa mara nyingine ameonyesha umahiri mkubwa katika nyanja hiyo.
Dk Ndumbaro ambaye ni daktari wa sheria, mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndiye alikuwa akimtetea Okwi katika kesi dhidi ya Yanga iliyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, jana.
Ndumbaro ambaye ni mwalimu wa katika Chuo Kikuu Huria (Out) aliwabana Yanga katika vipengele kadhaa na kuonyesha walivunja mkataba mapema.
Taarifa zinaeleza kutokana na Dk Ndumbaro kuibana sana Yanga, ilifikia wakati mwanasheria aliyekuwa upande wa Yanga aliamua kutoa hoja kadhaa zikiwemo barua zao walizoziwasilisha TFF kuhusiana na kuvunja mkataba wa Okwi na ikawa sehemu ya kosa kubwa ambalo daktari huyo wa sheria alitumia kumaliza kesi.
Mwanasheria huyo ambaye ni kati ya wanasheria wachache nchini kuwa madaktari wa sheria, alimpa wakati mgumu mwanasheria wa Yanga na kuibana Yanga katika vipengele hivi
Mwanasheria huyo ambaye ni kati ya wanasheria wachache nchini kuwa madaktari wa sheria, alimpa wakati mgumu mwanasheria wa Yanga na kuibana Yanga katika vipengele hivi
i) Yanga iliomba kuvunjwa mkataba wa Okwi bila ya kumpatia nakala, yeye akafanya juhudi ya kuzipata barua hizo na kukubaliana na hilo kwa barua pia, maana yake hakuwa tena na mkataba na Yanga.
ii) Yanga haikumalizia fedha zake dola 50,000 (Sh milioni 80), pia haikumlipa mshahara wa miezi mitano pamoja na nyumba, maana yake ilikiuka mkataba, hivyo ulishavunjika.
iii) Msisitizo bila ya kusema kiasi gani, Okwi naye anaidai Yanga fidia ya kukiuka mkataba ambao tayari umevunjika. Dk Ndumbaro ameitaka Yanga kumlipa mteja wake jumla ya shilingi milioni 111.8.
(Mchanganuo wa fedha hizo uko hivi; Fedha ya usajili dola 50,000 (Sh milioni 82.5), mshahara wa miezi mitano (kwa mwezi dola 3,000) dola 15,000 (Sh milioni 24.7) na kodi ya nyumba ya miezi 7, dola 400 kwa mwezi, jumla dola 2,800 (Sh milioni 4.6). Jumla ya zote ni Sh milioni 111.8.
Kutokana na ‘pini’ hizo za daktari huyo wa sheria maana yake, Okwi alikuwa huru, hivyo kamati hiyo inaweza kuendelea kujadili masuala mengine kuhusiana na ulipwaji wa fidia kutoka kwa kila upande kwenye kikao kingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment