Kiungo wa zamani wa Yanga, Athumani Iddi
Chuji na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki wamefeli majaribio ya
kucheza soka la kulipwa nchini Oman na imeelezwa sababu tatu ni chanzo.
Tayari Chuji na Mwombeki wametua jijini Dar wakiwa kwenye pipa la Oman Air ambalo limetokea katika jiji la Muscat kupitia Zanzibar.
Wawili hao pamoja na kiungo wa zamani wa
Simba, Jerry Santo wote wamefeli kuichezea timu ya Oman Club iliyo daraja la
kwanza.
Taarifa zinaeleza, Chuji ndiye pekee
alionyesha kiwango kizuri na ilibaki kidogo tu aingie mkataba na klabu hiyo
kongwe ya Oman.
Lakini katika mechi ya mwisho akashindwa
kuonyesha kiwango, hali iliyowafanya wahusika kuahirisha na kumuungaisha katika
kundi la Santo na Mwombeki.
Sababu tatu:
Moja:
Inaelezwa Santo na Mwombeki walionekana wazi
hawakuwa na stamina wala mazoezi ya kutosha.
Kwani walikuwa wanachoka mapema mazoezini
hali iliyoanza kumpa hofu kocha ingawa wao walilakamika kuhusiana na hali ya
hewa.
Mbili:
Mwombeki alionekana mzito sana wakati Santo
alishindwa kukaba labda kutokana na kutokuwa fiti. Chuji anaelezwa kujitahidi
katika mazoezi, huenda kwa kuwa alifanya mazoezi ya kutosha akiwa jijini Dar es
Salaam.
Tatu:
Walicheza mechi mbili za kirafiki, lakini
wakashindwa kabisa kuonyesha uwezo.
Chuji pekee ndiye alicheza mechi ya kwanza
vizuri na kuwapa matumaini viongozi wa Oman Club.
Santo na Mwombeki walishindwa kuanzia mechi
ya kwanza, ile ya pili ambazo zote timu yao ilitoka sare wakaharibu kabisa.
Chuji naye alifanya vizuri mechi ya kwanza,
lakini ile ya pili, kiwango kikawa chini.
TAARIFA:
Chuji na Santo walitaka kuendelea kubaki
Oman ili watafute timu nyingine, wakati Mwombeki alisisitiza kwamba anataka
kurejea nyumbani tu.
Hata hivyo ikashindikana, hivyo wote
wakalazimika kurejea mwakwao Tanzania na Kenya.
Mwombeki na Chuji wakaingia kwenye Oman Air
iliyopitia Zanzibar, wakati Santo akajitupia kwa Emirates ambayo imepitia Dubai
hadi Nairobi.
Hata hivyo hadi Chuji na Mwombeki wanaondoka
katika jiji la Muscat, Santo aliendelea kuwepo jijini Muscat na haikujulikana
kama kweli aliondoka au atapiga kona abaki na kuendelea kusaka timu.
0 COMMENTS:
Post a Comment