September 25, 2014



Mashabiki na wanachama mbalimbali wa Yanga, wamemuangukia Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu kuwa ndiye anahusika kusogezwa mbele kwa mechi ya watani iliyokuwa ipangwe Oktoba 12.
Mechi hiyo ya Yanga na Simba, imesogezwa na kesho itajulikana.

Mmoja wa wanachama wa Yanga, Yahaya Soud amesema ana hofu kubwa na Kaburu kwa kuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya TFF.
“Tuna hofu sana na Kaburu atakuwa amehusika, maana yeye yuko pia TFF na anashughulikia mashindano.
“Wanataka kuibeba Simba kwa kuwa sasa ina wachezaji majeruhi wengi, hivyo inataka wapone,” alisema.
Lakini Mbaraka Kibinda mkazi wa Sinza, naye amelaumu kuwa Simba wamefanya ujanja.
“Ni ujanja tu, wanajua hawako vizuri na kweli huyo Kaburu ninamhofia,” aliema.
Lakini SALEHJEMBE ilipompata Kaburu, alisema: “Hayo ni maneno ya kishabiki na watu wanapiga kelele.
“Kaburu ni mtu wa mpira ni lazima ataongoza mpira, angeweza kuwa kwenye kamati hiyo kiongozi wa Yanga au timu nyingine.
“Sasa nashangazwa na hao wanaolaumu, kwanza wajifunze kamati ya TFF haiandai ratiba, hiyo ni kazi ya bodi ya ligi,” alifafanua Kaburu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic