Katika jitihada za kumfanya awe tishio zaidi msimu
ujao, benchi la ufundi la Yanga limeamua kumuongezea programu ya mazoezi
straika Mbrazil, Genilson Santos ‘Jaja’.
Kuonyesha kwamba Yanga haitaki mchezo, Jaja
amekuwa akiendelea kufanyishwa mazoezi hata pale wenzake wanapopumzika.
Yanga, juzi Jumamosi asubuhi kwenye Uwanja wa
Shule ya Sekondari ya Loyola Mabibo jijini Dar, ilicheza mechi ya kirafiki
dhidi ya Polisi Dar iliyomalizika kwa bao 1-1.
Straika huyo aliendelea kukimbia kwa kuzunguka
uwanja kama alivyotakiwa na kocha wake, hali iliyowafanya mashabiki waamini
kuwa ni muendelezo wa mazoezi ya kumpa wepesi mchezaji huyo kabla ya ligi
kuanza Septemba 20, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment