September 1, 2014




Na Saleh Ally
SIMBA ndiyo mabingwa wa kwanza na wana rekodi ya kuuchukua ubingwa huo mara mbili mfululizo ikiwa ndiyo mwanzo tu wa Ligi Kuu Tanzania.


Simba wakati huo ikijulikana kama Sunderland, ilibeba ubingwa huo mwaka 1965, ikiwa ni mara ya kwanza kuanzishwa kwa ligi hiyo ikiwa imelenga kuipatia Tanzania mwakilishi kwenye Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Ghana, Kwame Nkurumah, kutoa kombe lililoanza kugombewa na klabu bingwa za Afrika.

Wakati klabu bingwa Afrika ilianza msimu wa 1962-63 na kufanyika Ghana, halafu 1964-65 iliyofanyika Tunisia, Tanzania haikuwa na mwakilishi kwa kuwa ligi haikuwa imeanzishwa.

Mwaka 1965, ikaanza na Simba wakawa mabingwa wapya na wa kwanza.
Bahati mbaya, Chama cha Soka Tanzania (Fat) kilichelewesha kupeleka majina kama mwaka uliofuatia, hivyo Simba hawakupata nafasi ya kushiriki.

Hata hivyo, lile kombe lililotolewa na Rais Nkurumah, lilianza kushindaniwa rasmi mwaka 1965, mwaka ambao Simba haikwenda licha ya kuwa bingwa wa Tanzania.

Ilipoanza ligi hiyo ilikuwa na timu sita tu zikiwemo Tobacco au Sigara (Pwani), Young African, Coastal Union na Manchester United (Tanga), TPC (Moshi) na mabingwa  Sunderland (Pwani).


Ubingwa wa kwanza, Simba iliupata bila ya kucheza baada ya Dar Young African, kuugomea mchezo kabla mwamuzi hajaumaliza  katika dakika ya 80 wao wakiwa wanaongoza bao 1-0.

 Fat ikaagiza urudiwe, Dar Young African wakaugomea na chama hicho  kikawatangaza wao ndiyo mabingwa.

Tokea kuanzishwa kwa ligi hiyo 1965, makombe 50 yametoka na hadi la msimu uliopita ambalo wamechukua Azam FC, ambao ni mara yao ya kwanza Simba wanashika nafasi ya pili.

Simba wanashika nafasi hiyo ya kubeba makombe mengi baada ya Dar Young African au Yanga waliochukua mara 24, halafu kikosi cha Msimbazi, mara 18, wengine ni Mtibwa Sugar mara mbili na timu zilizotwaa mara mojamoja kama Pan African, Cosmopolitan, Mseto, Tukuyu, Coastal Union na wanaochipukia, Azam FC.
Pia usisahau, Simba ndiyo mabingwa wa kwanza wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kagame na pia ndiyo wanaongoza kulitwaa mara nyingi zaidi, wamelibeba mara sita.
Miaka waliyolitwaa ni 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002.
Katika michuano mingine midogo ya Afrika Mashariki, Kombe la Tusker, Simba tena ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji hilo, mara nne kati ya michuano nane ya kombe hilo, katika miaka ya 2001, 2002, 2003 na 2005. Ililikosa mwaka 2006, lilipochukuliwa na Kagera Sugar, mwaka 2007, lilipochukuliwa na Yanga, mwaka 2008 lilipochukuliwa na Mtibwa Sugar na mwaka 2009, lilipochukuliwa na Yanga tena.

Asili ya Simba SC tangu enzi hizo ni kutandaza soka safi, la taratibu na kujiamini sana na si butubutu.

Kama kungekuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi makombe, basi kabati la Simba la kuhifadhia lingejaa ‘top’.
MAKOMBE RUNDO YA SIMBA:
UBINGWA WA LIGI KUU:
1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004 na  2007 (Ligi Ndogo), 2010 na 2012.
LILILOKUWA KOMBE LA NYERERE:
1984, 1995 na 2000
LILILOKUWA KOMBE LA MUUNGANO:
1993, 1994, 1995, 2001, na 2002
KOMBE LA TUSKER:
2001, 2002, 2003 na 2005
KOMBE LA CAF:
Ilifika fainali mwaka 1993
KOMBE LA KAGAME:
1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002
LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kucheza hatua ya makundi 2003
KLABU BINGWA AFRIKA:


ORODHA KAMILI YA MABINGWA WA LIGI KUU TANGU 1965:
1965 Sunderland (Simba)
1966 Sunderland (Simba)
1967 Cosmopolitan
1968 Yanga
1969 Yanga
1970 Yanga
1971 Yanga
1972 Yanga
1973 Simba
1974 Yanga
1975 Mseto
1976 Simba
1977 Simba
1978 Simba
1979 Simba
1980 Simba
1981 Yanga
1982 Pan Africans
1983 Yanga
1984 Simba
1985 Yanga
1986 Tukuyu Stars
1987 Yanga
1988 Coastal Union
1989 Yanga
1990 Simba
1991 Yanga
1992 Yanga
1993 Yanga
1994 Simba
1995 Simba
1996 Yanga
1997 Yanga
1998 Yanga
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba
2002 Yanga
2003 Simba
2004 Simba
2005 Yanga
2006 Yanga
2007 Simba
2007/08 Yanga
2000-09 Yanga
2009-10 Simba SC
2010-11 Yanga
2011-12 Simba SC
2012-13 Yanga
2013-14 Azam FC



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic