Kikosi cha JKT Ruvu, kitaanza Ligi Kuu Bara bila ya wachezaji wake saba wa kikosi cha kwanza.
Kocha
Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao ambao wamekwenda kushiriki michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki iliyokuwa ikifanyika mjini Zanzibar.
“Wachezaji wangu takribani saba wa kikosi cha
kwanza, hawapo kwa sasa, hili linanipa wakati mgumu sana, ligi inaanza siku ya
Jumamosi, uwepo wao una mchango mkubwa katika timu na wako Msumbiji kwa sasa
kulitumikia jeshi katika masuala la michezo.
“Lakini nitaendelea kupambana na msimu ujao
tunataka kuonyesha mabadiliko kwa kiasi kikubwa ili kuweza kufanya vizuri na siyo
kusuasua kama ilivyokuwa misimu ya nyuma,” alisema Minziro ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha msaidizi wa Yanga chini ya kocha Ernie Brandts raia wa Uholanzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment