NDANDA |
Betram Hamsini, Mtwara
Kikosi cha Ndanda cha mkoani Mtwara, leo
Jumatatu kinatarajia kuanza safari ya kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya
mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ya mkoani humo.
Ndanda inayodhaminiwa na matairi ya Vee Rubber ambayo juzi jumamosi ilitoka sare ya
0-0 na Simba katika mchezo wa kirafiki ulipigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
mkoani hapa, itafungua pazia la
Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Selemani Kachele,
alisema wanatarajia kuondoka leo kuelekea Shinyanga ambapo wamepeganga kuweka
kambi ya muda mfupi mkoani Morogoro.
“Timu inatarajia kuondoka leo kuelekea
Shinyanga tayari kwa ajili ya mechi yetu ya kwanza dhidi Stand United ila
tumepanga kuweka kambi ya muda mfupi Morogoro na tutafika huko siku moja kabla ya mechi.
“Kikikosi chetu kipo vizuri kwa ajili ya
mapambano ya ligi lakini pia naamini tunaweza kuibuka na ushindi kwa sababu
tumefanya maandalizi ya kutosha, ingawa katika mchezo lolote linaweza kutokea,”
alisema Kachele.
STAND UNITED SIKU WALIPOINGIA MKATABA NA MATAIRI YA DOUBLE STAR |
Stand pia inadhaminiwa na matairi bora ya Double Star na zote zimepanda daraja msimu huu zikitokea daraja la kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment