Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu
amesema kikosi chao kitafunga mabao mengi zaidi msimu huu.
Kavumbagu raia wa Burundi, amesema kikosi
chao ambacho safu yake ya ushambuliaji, kiungo na walinza wana ushirikiano
mkubwa, watafunga mabao mengi zaidi.
Akizungumza baada ya mechi dhidi ya Polisi, Kavumbagu alisema Azam FC ina ushirikiano wa juu, hali inayotoa nafasi karibu kila mchezaji kuwa na nafasi ya kufunga au kutoa pasi za mabao.
“Mimi ninaamini tutafunga mabao mengi zaidi.
Washambuliaji tunaelewana vizuri na viungo.
“Bado utaona kwa Azam hata mabeki wanaweza
kufunga, subiri ligi inaendelea utakubali ninachosema,” alisema Kavumbagu.
Mrundi huyo aliyekipiga Yanga msimu uliopita
ameanza ligi kwa kupachika mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Polisi
Moro iliyopanda daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment