Hali imeonekana kuwa nzurio kutokana na
Manchester United kuendelea kuboronga na safu yake ya ulinzi kuwa nyanya.
Mechi iliyopita Man United imefungwa mabao
5-3 na Leicester City ikiwa ni bada ya kuongeza kwa mabao 3-1.
Picha unayoiona, inaonyesha kiasi gani safu
yake ya ulinzi inacheza shaghalabagala. Wachezaji hawakai katika sehemu zao.
Angalia aliyewekewa namba 2, huyo ni
Blackett ambaye ameamua kubaki nyuma peke yake bila ya kuangalia wenzake
wamejipanga vipi.
Ukiachana na hivyo, katika picha hiyo kuna
wachezaji saba wa Man United na watatu tu wa Leicester City lakini bado
waliweza kuleta madhara.
Kitu kikubwa cha tatu, katika wachezaji saba
wa Man United, hakuna hata mmoja aliyemkaba mchezaji mmoja tu kati ya watatu wa
Leicester City.
Hayo ndiyo sehemu ya madudu ya safu ya
ulinzi ya Man United.
0 COMMENTS:
Post a Comment