PHIRI AKIWA MAZOEZINI ZANZIBAR. |
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri
amesisitiza wachezaji kusahau kuhusiana na mechi waliyotoka sare ya mabao 2-2
dhidi ya Coastal Union.
Phiri ametaka wachezaji wake kujifunza
kupitia mchezo huo na wayarekebishe wakati watakapokutana na Polisi Moro,
Jumamosi.
“Kukumbuka makosa ni jambo zuri kwa ajili ya
kurekebisha, kila siku zinavyokwenda unatakiwa kupunguza kiwango cha kusahau.
“Halafu unaweka nguvu nyingi kwenye mafunzo
kwa ajili ya kurekebisha kosa ulilofanya.
“Tuikuwa na mengi tuliyokosea, sawa walinzi
walifanya uzembe, lakini washambuliaji pia walipoteza nafasi muhimu.
“Kuna wakati viungo pia walikosea jambo nah
ii ndiyo maana ya timu,” alisema Phiri na kuongeza.
“Sasa ni wakati wa kujirekebisha na siku ya
mechi ijayo, tufanye kazi bora zaidi.”
Simba iko Zanzibar imeanza kazi kwa ajili ya
kujiwinda kuwavaa Polisi Moro ambayo itakuwa ni mechi yake ya pili.
Katika mechi dhidi ya Coastal, Simba
ilitangulia kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, kipindi cha pili, Coastal ikarudisha
yote na kuwapa presha kubwa ikikaribia kufunga la tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment