Gareth Bale, Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na James
Rodrigues walikuwa kati ya waliochangia mabao hayo matano.
Liverpool nayo ikiwa imerejea tena kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuikosa kitambo, ilifanikiwa kuibuka na
ushindi.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ludogorets,
Liverpool ikiwa nyumbani Anfield Mario Balotelli na nahodha Steven Gerrard
aliyefunga mkwaju wa penalti katika dakika ya 90 ndiyo walikuwa mashujaa wa
leo.
Lakini ilikuwa bahati mbaya kwa Arsenal
iliyokuwa ugenini nchini Ujerumani dhidi ya Borussia Dortmund ambayo iliwapa
kichapo cha mabao 2-0.
Waliowauwa Arsenal ni Ciro Immobile na
Aubameyang na juhudi za vijana wa Wenger hazikufanikiwa angalau kupata bao la
kufutia machozi.
Juventus wakiwa nyumbani, wakaifunga Malmo
ya Sweden kwa mabao 2-0 na Benfika ikiwa nyumbani pia ikalala kwa mabao 2-0
dhidi ya Zenit.
Galatasaray ikiwa Istambul, ikashikiliwa kwa
sare ya bao 1-1 dhidi ya Anderlecht ya
Ubelgiji. Monaco ya Ufaransa ikajitutumua kwa kuichapa Bayer Leverkusen
kwa bao 1-0 lililofungwa Joao
Moutinho.
Olimpiako nayo ikawashangaza wengi, ikiwa
nyumbani ikawachapa wabishi Atletico kwa mabao 3-2 katika mechi safi yenye
ushindani mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment