Kitendo cha kubadilishana jezi
kilichofanywa na viungo washambuliaji, Mrisho Ngassa wa Yanga na Salum Abubakar
‘Sure Boy’ wa Azam FC, katika mechi ya Ngao ya Jamii, kilikuwa ni danganya toto
kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo.
Mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo,
waliwashuhudia viungo hao wakibadilishana jezi wakati wa mapumziko walipokuwa
wakielekea vyumbani, kitendo ambacho kilipongezwa na wengi kuwa ni uungwana.
Timu hizo zilikutana Jumapili iliyopita kwenye
Uwanja wa Taifa katika mechi ya Ngao ya Jamii ambapo Yanga ilishinda kwa mabao
3-0.
Ofisa Habari wa Azam, Jaffari Iddi alipoulizwa
juu ya kitendo hicho alifunguka kwa kusema: “Tukio hilo lilifanyika kwa ajili
ya kuonyesha michezo ni upendo lakini kila mmoja alichukua jezi yake walipofika
katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo. Lilikuwa tukio zuri la kuonyesha
uungwana na upendo baina ya timu hizo.”
Kitendo cha wachezaji hao kubadilishana jezi
wakati wa mapumziko kiliwashitua mashabiki wengi wa soka.
Huenda walianza kuhisi kuwa tukio kama lile la
misimu miwili iliyopita wakati Ngassa akiwa Azam FC halafu akachukua na kuibusu
jezi ya Yanga, litajitokeza tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment