Na Saleh Ally
KWA miaka kumi sasa tokea
2004, inaonekana kumekuwa na mchuano mkali sana katika suala la ufungaji mabao
kwenye Ligi Kuu Bara.
Awali ilionekana kama
washambuliaji kutoka nyumbani wamelala kwa kuwa wageni wanatawala zaidi kila
unapofika mwisho wa msimu na hesabu kupigwa nani ni mfungaji bora.
Tokea mwaka 2004 ni misimu
kumi, wenyeji wamekuwa wafungaji bora mara tano, sambamba na wageni.
Maana ya yake msimu huu
mpya, itakuwa ni fainali, kuwa katika kipindi cha miaka 11, iwapo atashinda
mwenyeji, watakuwa wamewashinda wageni au wakishinda wao, wenyeji watakuwa wameangushwa.
Bado wenyeji wanashikilia
rekodi ya mabao mengi zaidi, msimu wa 2006-07, Abdallah Juma aliyekuwa
anakipiga Mtibwa Sugar, alipiga mabao 40. Hakuna mgeni wala mwenyeji aliyefikia
idadi hiyo.
Boniface Ambani (Yanga),
John Bocco (Azam FC) na Amissi Tambwe wa Simba, msimu uliopita ndiyo walijaribu
kumkaribia baada ya kufikisha mabao 19.
Bado wachezaji wenyeji wana
changamoto kubwa kwa kuwa kwa misimu miwili sasa wafungaji bora wa Ligi Kuu
Bara wametokea nje, Kipre Tchetche-Ivory Coast na Tambwe-Burundi.
Watakubali wageniw apige
‘hat-trick’ ya ufungaji bora, au mmoja atakataa na kuibuka na nafasi hiyo?
Inawezekana lakini
haitakuwa kazi lahisi, angalia Simba ina watu kama Paul Modo Kiongera, Emmanuel
Okwi na Tambwe.
Cheki Yanga ina mambo
mapya, Wabrazil wawili, Jaja na Coutinho ambao wameanza kuonyesha wana kitu
fulani. Hivyo haitakuwa kazi lahisi na ushindani wao utavuta mengi.
Washambuliaji na viungo wa
kigeni wamekuwa wakitaka kuonyesha umuhimu wao kuwa fedha nyingi kutumia dola
ambazo wamekuwa wakilipwa, wanastahili.
Lakini wanasaidia kuleta
changamoto kubwa kwa wenyeji ambao wanataka kuonyesha kinachofanywa na wageni
wala si ishu, wao pia wako fiti.
Ligi Kuu Bara inaanza rasmi
leo, viwanja vitawaka moto kila timu ikitaka kuanza na mguu bora wa kwanza.
WAFUNGAJI BORA TANGU 2004:
Mwaka Nchi Mfungaji Timu Mabao
2004/05 Tanzania Abubakar Mkangwa Mtibwa 16
2005/06 Somalia Cisse
Abshir Simba 19
2006/07 Tanzania Abadallah
Juma
Mtibwa 20
2007/08 Uganda Mike Katende Kagera
11
2008/09 Kenya
Boniface
Ambani Yanga 18
2009/10 Tanzania
Mussa Mgosi Simba 18
2010/11 Tanzania
Mrisho Ngassa Azam 18
2011/12 Tanzania John Bocco Azam 19
2012/13 Ivory Coast Kipre Tchetche Azam 17
2013/14 Burundi Amissi Tambwe Simba 19









0 COMMENTS:
Post a Comment