Kungo Shinji Kagawa ameanza kuonyesha kuwa
bado yuko safi licha ya kuonkana hana kiwango cha juu akiwa Man United.
Kagawa amefunga bao moja na kutoa pasi
iliyozaa bao wakati Borussia Dortmund ilipoilaza Freiburg kwa mabao 3-1 katika
Bundesliga.
Katika mechi hiyo, Dortmund wakiwa nyumbani
walionyesha kiwango kizuri dhidi ya timu hiyo kutoka Kusini mwa Ujerumani.
Adrian Ramos alianza kufunga bao la kwanza
katika dakika ya 34, Kagawa akafunga la pili katika dakika ya 41.
Lakini Kagawa tena akatoa pasi safi kwa
Aubameyang aliyefunga la tatu katika dakika ya 78.
Wageni Freiburg walipata bao lao la kufutia
machozi katika dakika ya 90 kupitia Oliver Sorg.
0 COMMENTS:
Post a Comment