Pamoja na Real Madrid kuwa na kikosi ghali,
watani wao Atletico Madrid wameendeleza ubabe dhidi yao baada ya leo kuwachapa
mabao 2-1 wakiwa kwao Santiago Bernabeu.
Licha ya kucheza bila ya kocha wake, Diego Semone, Atletico ilionyesha soka safi na Thiago na Arda ndiyo walifunga mabao hayo mawili huku lile la kufutia machozi likipachikwa na Ronaldo.
Kipindi cha pili kilionekana zaidi kuwa cha
wageni na wangekuwa makini wangeweza kupata mabao mengi zaidi.
Licha ya kujaza vijana wengi mbele kama
James Rodrigues, Isco na Javier Harnandez, Madrid haikufua dafu kwa Atletico
ambayo katika mechi ya Super Cup pia iliwatwanga.
Mechi ya leo ya La Liga ni ya pili kwa
Madrid kupoteza, hali inayomuweka kwenye wakati mgumu kocha wake Carlo
Ancelotti.
0 COMMENTS:
Post a Comment