Bondia Floyd Maywether
ameendeleeza ushindi kwa mara ya pili dhidi ya Marcos Maidana.
Katika pambano lililoisha punde,
Mayweather ameibuka mshindi kw apointi baada ya majaji wote watatu kumpa
ushindi mnono.
Majaji hao watatu walitoa
ushindi wa 115-112, 116-111 na 116-111 kwa Mayweather katika pambano hilo
lililopigwa MGM Las Vegas, Marekani.
Tofauti na pambano la mwanzo, Mayweather
alionekana kuwa fiti zaidi na kutawala ingawa alionekana kuwa makini sana.
Maidana ambaye ana ngumi kali
zaidi, alionekana si yule aliyekuwa tishio katika pambano la mwanzo.
Hata hivyo alimpa wakati mgumu Mayweather
katika raundi ya tano ambayo aliishika vizuri.
Mayweather alilalamika kuubwa
kwenye glavu yake wakati wamekumbatiana na na Maidana.
Pamoja na picha kuonyesha
Maidana akiuma, yeye aliendelea kusisitiza kwamba hakuuma.
Mwisho Mayweather alimsifia kuwa
ni bondia bora lakini akasisitiza yeye ataendelea kuwa namba moja.
Kwa ushindi huo, Mayweather
amefikisha rekodi ya mapambano 47 na kushinda yote, katika hayo 26 kwa KO na usisahau ana miaka 37.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment