Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema kamwe hajawahi
kuonyesha dharau kwa Yanga kwamba ni timu lahisi.
Lakini akasisitiza, hakuwahi wala hataiogopa Yanga hata siku
moja, badala yake atafuata misingi ya kazi yake.
Phiri raia wa Zambia ameiambia SALEHJEMBE kuwa, kocha makini
hawezi kuhofia kitu, badala yake anajipanga.
“Dharau ni sehemu ya kutoka nje ya mfumo sahihi ya kocha bora.
“Kocha bora anajipanga kushinda na si kushindwa. Ukidharau maana
yake unapotea na inaweza kuwa lahisi kushindwa.
“Yanga ni moja ya timu kubwa, kongwe na zenye mafanikio hapa
Tanzania. Siwezi kuidharau hata kidogo.
“Badala yake ninaheshimu wanachofanya na tunapokaribia kukutana
nao, najiandaa vizuri kutokana na ninavyowajua,” alisema Phiri ambaye alikuwa
uwanjani wakati Yanga inaivaa Azam FC na kuichapa kwa mabao 3-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment