September 4, 2014


Utamu wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Simba dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Jumamosi umezidi kuongezeka.

Utamu huo umezidi baada ya Gor Mahia kueleza kwamba mashabiki wake wakiwa kwenye mabasi matano wanaondoka Nairobi kuja Dar es Salaam kuishangilia timu yao katika mechi hiyo hiyo dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa.

"Kweli wanakuja wakiwa kwenye mabasi matano, hivyo watawapa wakati mgumu mashabiki wetu, lazima wajiandae.
"Mashabiki wa Gor Mahia hushangilia mwanzo mwisho na wanajulikana kama mashabiki namba moja nchini Kenya," alisema Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Hiyo itakuwa ni mechi ya kwanza ya Simba ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa chini ya Patrick Phiri kwa mara nyingine.
Simba imekuwa kambini kisiwani Unguja ambako imecheza mechi tatu na kushinda zote.
Mechi yake ya mwisho dhidi ya KMKM, ilishinda kwa mabao manne huku ikionyesha soka safi na la kuvutia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic