Juhudi za Yanga kuipata APR ya Rwanda kwa ajili ya mechi yake ya pili ya kimataifa ya kirafiki, zimekwama.
Sasa Yanga itacheza na Big Bullets ya Malawi.
Mechi ya kirafiki dhidi ya timu hizo inatarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Awali Yanga ilitangaza kucheza na APR lakini hali hiyo imekuwa ngumu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema watacheza na Big Bullet zamani ikiwa inajulikana kama Bata Bullet.
"Kweli sasa tutacheza na Wamalawi ambao tayari watakuja nchini kwa ugeni DRFA," alisema Njovu.
"Sisi tunaendelea kujiandaa tukisubiri mechi hiyo kwa ajili ya kujipima tena."
Kwa mara ya kwanza, Yanga chini ya Marcio Maximo wameshinda mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Thika United ya Kenya kwa kuwafunga bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment