Baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi
mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga huku Mbrazili mmoja, Geilson Santos ‘Jaja’
akiwemo dimbani, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amewaponda Wabrazili
wa Yanga akisema ni wachezaji wa Uwanja wa Taifa tu.
Mtibwa iliendeleza ubabe wake kwa Yanga kwenye
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, juzi mbele ya mashabiki kibao waliojitokeza,
shukrani kwa mabao ya mkongwe Mussa Mgosi na Ame Ali.
Lakini baada ya mchezo huo, Maxime ambaye
alimfunga kocha wake wa zamani wa Taifa Stars, Marcio Maxime, alisema Jaja na
Coutinho watapata tabu sana watakapokuwa wakicheza kwenye viwanja vya mikoani
kutokana na kuwa vibovu.
Alisema katika mechi yao, Jaja alipata wakati
mgumu sana kucheza kutokana na uwanja kuwa mbovu lakini kama angekuwa akicheza
kwenye Uwanja wa Taifa, pengine angefanya maajabu kama ilivyokuwa dhidi ya Azam
katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Jaja alikosa penalti ambayo ingeweza kuipatia
Mtibwa bao la kusawazisha.
“Jaja siyo mbaya ni mchezaji mzuri sana ila
viwanja vya Tanzania vitamsumbua sana, mpaka aje kukaa sawa itamchukua muda mrefu.
“Kwa jinsi ninavyoona mchezaji huyo na mwezake
watakuwa wakifanya vizuri tu watakapokuwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa sababu ni
mzuri ukilinganisha na hivi vya mikoani, ambavyo wachezaji wetu wamevizoea,”
alisema Maxime.
0 COMMENTS:
Post a Comment