VIONGOZI WA MBEYA CITY WAKIWA PAMOJA NA MMOJA WA VIONGOZI WA KAMPUNI YA BIN SLUM TYRES, SIKU WALIPOINGIA MKATABA WA UDHAMINI. |
Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya inayodhaminiwa na kampuni ya Bin
Slum Tyres Ltd kupitia betri zake za RB imeamua kurudisha faida inayopata kwa
jamii ambapo imesema imepanga kuwasomesha watoto 100 wenye ulemavu katika shule
mbili za Itigi na Iyole.
Ofisa Habari wa Mbeya City ambaye ameanza kazi rasmi Septemba Mosi,
mwaka huu, Dismas Ten, ameliambia gazeti hili kuwa, mikakati yote ya zoezi hilo
inaendelea vizuri.
“Kati ya wanafunzi hao wa kike ni 45 na wa kiume 50 ambao
tutawaendeleza hadi watakapomaliza shule, kila kitu kinakwenda sawa kuhusiana
na suala hilo,” alisema Ten.
Mbeya City ilipanda ligi msimu uliopita na kufanikiwa kufanya vema
hadi kushika nafasi ya tatu.
Pamoja na kushika nafasi hiyo, Mbeya City ilikuwa kiboko ya vigogo
ikizitikisa Simba, Yanga na Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment