Ushindani wa Ligi Kuu Bara umeanzia kwenye maneno hata kabla ya timu
kuingia uwanjani baada ya tambo na kubezana kuanza mapemaa.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amewaponda amesema akidai
wala hawana hofu kwa kuwa Simba haijafanya usajili wowote wa maana na ndiyo
maana inaogopa kucheza mechi ya kirafiki dhidi yao.
Awali Simba ilikuwa icheze na Mtibwa Sugar lakini ikaamua kuandaa
mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia, kesho.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya Simba kukataa kucheza na Mtibwa
katika mchezo maalum wa kufanya majaribio ya tiketi za kielektroniki, uliokuwa
upigwe leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa.
Kifaru alisema Simba waliogopa muziki wao kwa kuwa usajili wao hauna
lolote na kudai kuwa wachezaji wao wapya wakiwemo Paul Kiongera raia wa Kenya na
Pierre Kwizera kutoka Burundi ni sawa na wafanyabiashara wa mitumba na siyo
wachezaji hatari.
“Mtibwa siyo timu ndogo ndiyo maana Simba wameogopa, hao wachezaji
wao wapya ni wauza mitumba. Mimi siamini kama ni wachezaji wa kimataifa.
Wanatudanganya tu, wanatuletea watu wa mitaani, wanasema ni wachezaji,” alisema
kwa kujiamini.
Simba, imepanga kujipima dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor
Mahia, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
0 COMMENTS:
Post a Comment