KIKOSI CHA NDANDA FC. NDIYO TIMU ILIYOANZA KWA USHINDI WA MABAO MENGI ZAIDI. |
Ligi Kuu Bara liyoanza kutimua vumbi wikiendi
iliyopita ilishuhudiwa michezo saba ikipigwa kwenye viwanja tofauti, ambapo
mabao yalipatikana kwa kila mechi lakini mchezo mmoja tu uliisha kwa sare ya
kutofungana uliowakutanisha Mbeya City dhidi ya JKT Ruvu.
Katika michezo hiyo, mabao 18 yaliingia wavuni
ambapo idadi hiyo ni pungufu ya bao moja kama ukilinganisha na michezo ya awali
ya msimu uliopita.
Matokeo ya michezo hiyo ni Ndanda 4-1 Stand
United, Azam 3-1 Polisi Moro, Mtibwa 2-0 Yanga, Ruvu Shooting 0-2 Prisons,
Mgambo 1-0 Kagera Sugar, Mbeya City 0-0 JKT Ruvu na Simba 2 – 2 Coastal Union.
Msimu uliopita katika michezo ya kwanza ya
ligi, yalifungwa jumla ya mabao 19 ambapo mwisho wa msimu timu ya Azam iliibuka
bingwa wa ligi hiyo.
Mchezo kati ya Stand United ikichapwa mabao 4-1 dhidi ya Ndanda FC ndiyo uliokuwa na mabao mengi zaidi kuliko michezo mingine yote.
0 COMMENTS:
Post a Comment