GLOBAL FC... |
Timu ya Global FC ambayo imeshinda mechi nne
mfululizo za kirafiki, leo Jumatano inatarajiwa kujitupa uwanjani kupambana na
timu ya Wizara ya Katiba na Sheria katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye
Uwanja Mawasiliano, Ubungo jijini Dar.
Mkurugunzi wa Habari na Mawasiliano wa Global
FC, Nassor Gallu,amesema mbali na mchezo huo wa
soka, pia kutakuwa na michezo mingine ikiwemo kuvuta kamba baina ya timu hizo,
lengo likiwa ni kuboresha uhusiano na kuimarisha afya.
“Siku ya Jumatano (leo) tutakuwa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya wenzetu wa Wizara ya Katiba ambao wanajiandaa na mashindano
ya Shimiwi. Lakini jambo jema ni kwamba mbali na soka, pia kutakuwa na mchezo
wa kuvuta kamba.
“Lengo ni kujiimarisha kiafya na kuboresha
uhusiano maana michezo ni furaha. Kikosi chetu kipo vizuri, kwa hiyo niwaomba
mashabiki waje kwa wingi kushuhudia burudani hiyo,” alisema Gallu.
Timu ya Global imekuwa ikicheza mara kwa mara
michezo ya kirafiki ambapo Ijumaa ya wiki iliyopita, ilikipiga na Shein Rangers
na kutoka nao suluhu.
0 COMMENTS:
Post a Comment