Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta
amefunguka kuwa uwepo wa Ugonjwa wa Ebola kwa nchi za Afrika siyo habari njema
hasa kisoka.
Hivi karibuni iliripotiwa kuwa ugonjwa huo tishio zaidi kwa
sasa umeingia nchini humo lakini yeye amepinga kuwa bado haujafika.
Straika huyo alisema
kuwa anauogopa ugonjwa huo ambao ni hatari sana na unatishia maendeleo ya soka
baada ya baadhi ya mechi kusitishwa huko Afrika Magharibi.
“Ugonjwa wa Ebola umekuwa tishio sana katika bara letu
la Afrika, yaani naogopa sana licha ya kuwa kwetu bado haujafika, naomba Mungu
usije kwani unarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Ingawa hata Congo kulikuwa kunahisiwa kuwepo kwa
mlipuko wa ugonjwa huo lakini haijathibitishwa rasmi, natoa pole kwa waathirika
kwa sababu ugonjwa huu unazuia mambo mengi ya maendeleo,” alisema Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment