Simba imeshindwa kuwapata AS Vita kutokana na wachezaji wake nane kubanwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo.
Kutokana na hali hiyo, imeamua kuwaagiza wababe wake, URA ya Uganda.
URA wanatarajia kuwasili leo kwa ajili ya kuwavaa Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
URA ina rekodi ya kuitambia Simba kila wanapokutana katika mechi za kirafiki au mashindano.
Hivyo katika mechi hiyo ya kirafiki ya kesho, Simba itakuwa na kasi ya 'kuitoboa' ngome ya URA ambayo huwa 'inaitesa' Simba inavyotaka yenyewe.
0 COMMENTS:
Post a Comment