Wakati nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
alitoa kibendera kidogo kama sehemu ya kuonyesha uanamichezo kwa nahodha wa
Mtibwa Sugar, Shabani Nditi, yeye hakuwa na lolote.
Kawaida timu hubadilishana bendera hizo
ndogo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha uanamichezo ni upendo na ushirikiano.
Katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara
mjini Morogoro, Jumapili, Cannavaro kwa niaba ya Yanga, alimkabidhi Nditi.
Baada ya hapo, Nditi hakuwa na lolote la
kutoa na baada ya hapo aliishia kumpa mkono Cannavaro.
Nditi hapaswa kulaumiwa, lakini klabu
kupitia viongozi wao kwa mfano huo wa Mtibwa Sugar zinapaswa kujirekebisha na
kuangalia mambo kama hayo.
Kwani kibendera hicho ni kiasi gani, mechi
wanazocheza ni 26, sasa vipi washindwe kuwa navyo?
Inawezekana likaonekana ni jambo dogo sana
lakini kwa uhalisia si jema na itakuwa vizuri kila timu ikaikabidhi nyingine
kibendera kuonyesha au kukamilisha maana hiyo ya ushirikiano.
Kama upande mmoja tu unaweza kufanya,
mwingine usitoe chochote zaidi ya mkono, dhana haiwezi kutimia.
Mtibwa wamefeli kwenye hilo katika siku ya
kwanza, lakini wanaweza kurekebisha mambo katika mechi zao zinazofuata na
wengine pia wakafanya hivyo, ndiyo ligi inakua hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment