| PHIRI AKIBONGA NA SALEH ALLY NA KUELEZA ALIVYOFURAHISHWA NA KAZI YA SALEHJEMBE. |
Phiri amesema familia na marafiki zake wamekuwa wakimfuatilia na kujua maendeleo yake ingawa bado wanasumbuka kidogo na Kiswahili.
"Wako wanaelewa Kiswahili kiasi fulani, lakini wengi bado ni shida. Ila wananieleza wanaona picha na pia ni lahisi kujua ninachofanya.
"Kazi nzuri, najua inahitahi kujituma na muda mwingi, lakini usikate tamaa, huenda baadaye ikawa blogu kubwa duniani," alisifia Phiri baada ya kukutana na mmiliki wa Blog hii, Saleh Ally Neke ambaye ni mwandishi mkongwe wa michezo kitaifa na kimataifa.
Akizungumzia pongezi hizo, Saleh Ally Neke aliwapongeza wadhamini na wasomaji wa Salehjembe kuwa wamekuwa changamoto kwake.
"Nimemshukuru Phiri, lakini wasomaji na wadhamini ni changamoto kubwa. Mwanzo nilianza kama sehemu ya kujiburudisha.
"Lakini sasa, kazi inazidi kupamba moto kwa kuwa sitaki kuwaangusha wadhamini na wasomaji wangu.
"Niko busy sana, lakini najitahidi kadiri ya uwezo wangu kwa kiasi kikubwa na hujisikia faraja nikiona watu angalau wanaridhika," alisema.
Kabla ya Phiri kutua nchini, kwa siku ni wasomaji 1200 hadi 2500 tu kutoka Zambia walikuwa wakifuatilia SALEHJEMBE, lakini sasa imepanda hadi kufikia kuanzia wasomaji 4500 hadi 6000 kwa siku.
Blog hii inadhaminiwa na Sapphire Court Hoteli, Samsa Real Estate, Bin Slum Tyres Ltd, Kiwango Security, Bambi na KD Hotel.







0 COMMENTS:
Post a Comment