Ronaldinho amekumbana na kitendo cha ubaguzi wa rangi kutoka kwa
mwanasiasa mmoja nchini Mexco.
Mwanasiasa huyo kutoka chama cha PAN amembagua Ronaldinho
akimfananisha na sokwe.
Sababu kubwa ya kumbagua ni kutokana na foleni kubwa ya magari
barabarani iliyosababishwa na mashabiki wa timu ua Querétaro aliyojiunga nayo
nchini Mexico.
Wengi walikuwa wanatokea uwanjani wakati Ronaldinho
anatambulishwa.
Mwanasiasa huyo akaamua kuandika kwenye ukurasa wake wa
Facebook, kama anachukizwa na mchezo wa soka na anashangazwa watu kusababisha
foleni sababu ya sokwe mmoja.
Kauli hiyo ilipingwa na wengi na kusababisha mwanasiasa huyo
aliyewahi kuwa waziri kuifuta post yake.
Hata hivyo, watu wameendelea kumsakama na kupinga kitendo chake
hicho cha kibaguzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment