Kocha Mkuu Prisons, David
Mwamwaja ameonyesha hofu kuhusiana na mshambuliaji wa Yanga, Jaja raia wa Brazil
kwamba asipewe upendeleo maalum
kwa maana ya kulindwa bila sababu.
MWAMWAJA AKIWA NA KIKOSI CHA PRISONS |
Mwamwaja ambaye ni mmoja
wa makocha wazoefu amesema kikosi chake kiko imara na tayari kwa ajili ya mechi
dhidi ya Yanga Jumapili jijini Dar, lakini asingependa kuona kuna upendeleo
fulani kwa wachezaji, mfano akieleza kuhusu Jaja.
“Kwa kweli sisi
tumejiandaa, umeona mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Ashanti pia imetusaidia,
kuna mambo ya kujifunza na kurekebisha.
“Lakini vizuri
uchezeshaji uwe mzuri na haki, kusiwe na upendeleo wa wachezaji fulani
kuonekana kama wao ni tofauti.
“Silengi kuwalaumu
waamuzi, ila natoa tahadhari mapema kwamba sisi hatuna hofu na Jaja wala
mchezaji mwingine wa Yanga, tumejiandaa kucheza vizuri na kutafuta ushindi,”
alisema Mwamwaja akionyesha kujiamini.
Prisons ilishinda mchezo wake wa kwanza wa Ligi
Kuu bara kwa kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 2-0, wakat Yanga ilipoteza kwa idadi
hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment