Uongozi wa Azam FC
umesema nafasi ya kocha wake wa timu ya vijana, Vivik Nagul aliyerejea kwao India utazibwa na makocha kati ya wanane.
Lakini ukafafanua kwamba
hakuna kocha ambaye ameishapata nafasi hiyo, badala yake Kocha Mkuu wa Azam FC,
Joseph Omog ameachiwa nafasi ya kuangalia nani atafanya naye kazi.
“Kweli kuna makocha
wanane ambao ndiyo tunaangalia kati ya hao, nani azibe nafasi ya Nagul.
“Nimesikia magazeti
yanaandika (Patrick) Liewig kutoka Ufaransa ndiye tumemuajiri. Ukweli abdo na
Omog ataamua.
“Baada ya hapo ndiyo
tutatangaza, lakini sasa bado uamuzi wa mwisho haujafikiwa,” alisema Mwenyekiti
wa Azam FC, Said Mohammed.
Nagul ameamua kurejea
kwao baada ya kupata dili la kuifundisha timu moja nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment