Taifa Stars imeambulia kipigo cha mabao 2-0
katika mechi yake ya kirafiki iliyomalizika hivi punde mjini Bujumbura.
Hii ni mara ya pili Stars inafungwa na
Warundi hao ambao ndani ya mwezi mmoja tu na ushee, waliifunga Stars mabao 3-0
jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya leo ya kupandisha
viwango, Burundi ilipata mabao yote yalipatikana katika kipindi cha kwanza.
Bao la kwanza lilifungwa na Saido
Ntibazonkiza katika dakika ya kwanza tu.
Bao la pili lilifungwa na Yusuf Ndikumana ‘Lule’
katika dakika ya 29.







0 COMMENTS:
Post a Comment