Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeanza kusikiliza kesi inayomhusu
mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kesi hilo inasikilizwa kwenye hoteli ya
kitalii ya Colosseum ya jijini Dar es Salaam.
Habari zinaeleza kuwa kuna mvutano mkali wa
kisheria kuhusiana na kesi hiyo ambayo Yanga na Simba zinamgombea Okwi raia wa
Uganda.
Yanga inaeleza bado ni mchezaji wake na ina
mkataba naye ingawa imemfungulia madai TFF ikitaka kuvunja naye mkataba na
afungiwe, pia alipe kitita cha faini ya Sh milioni 700. Kati ya hizo milioni
200 kwa ajili ya kuzungumza na timu ya Misri akijua ana mkataba na milioni 500
kuingia mkataba na Simba wakati akijua ana mkataba na Yanga.
Lakini Simba imemsainisha mkataba wa miezi
sita kwa kuwa ameomba imsitili kipaji chake kwa kuwa Yanga imeandika barua ya
kuvunja mkataba naye akasema sawa.
Kesi hiyo ndiyo inaendelea sasa na huenda
leo majibu yakapatikana kama ukali wa mvutano hautazidi kupanda juu.







0 COMMENTS:
Post a Comment