September 15, 2014

 Yule shabiki maarufu kama Steve wa Kulia, naye alikuwa uwanjani wakati Yanga ikiitwanga Azam FC kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana.

Kwenye picha hapo juu utafikiri anamueleza mwenzake kuwa "yule Jaja ni noma sana."
Steve alikuwa shabiki mkubwa wa Yanga na aliangua kilio kikubwa wakati Yanga ilipokumbana na dhoruba ya mabao 5-0 kutoka kwa Simba.
Lakini hivi karibuni akatangaza kuhamia Azam FC kama unavyomuona.
Mara tu baada ya kutua Azam, amekutana na Yanga iliyo sawa, ikaikung'uta Azam FC 3-0.
Swali, Steve kweli amehamia Azam FC kwa moyo wote au kipigo hicho kitamshawishi kurejea "nyumbani kwao"? Acha tungoje.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic