Kikosi cha DR Congo
kimepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan hivyo kuongoza kundoi A baada ya
Nigeria kunazwa kwa sare ya bila mabao na Afrika Kusini katika mechi iliyopigwa
jijini Cape Town.
Mshambuliaji mpya wa Everton,
Christian Atsu aliisadia Ghana kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Togo baada
ya kufunga bao katika dakika ya 85.
Kumbuka mechi ya kwanza,
Ghana wakiwa nyumbani walibanwa kwa sare ya suluhu dhidi ya Uganda.
Timu hiyo ya Afrika
Mashariki imeendelea kushangaza baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea
ikiwa nyumbani kwao.
Uganda inayoongozwa na
kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojevich ‘Micho’ sasa ndiyo inaongoza Kundi
E.
2-0 at home.
Nayo timu kutoka visiwa
viduchu vya Cape Verde imeendelea kuweka juu matumaini yake ya kufuzu katika
Kombe la Mataifa Afrika litakalopigwa Morocco baada ya kuiangusha Zambia
iliyosafiri hadi Magharibi kabisa mwa bara la Afrika.
Misri ambao ndiyo mabingwa
mara saba wa Kombe la Mataifa Afrika, wameendelea kuwa nyanya baada ya kuchapwa
bao 1-0 na wapinzani wao Tunisia wakiwa nyumbani Cairo.
0 COMMENTS:
Post a Comment