Mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi ameapa kuwa siku chache zijazo waliosema "Okwi mwisho Chalinze, kila mtu mjini Jaja", hawatarudia kusema hilo.
Okwi ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.
Okwi ameonyesha kusikitishwa na ujumbe huo ambao umekuwa ukisambaa kwa kasi kubwa.
Akasisitiza kuwa amerejea Simba ambako yeye ni nyumbani na watu wanapaswa kumuamini.
Anachohakikisha kuwa msemo huo utafutika kutokana na atakavyoitumikia Simba kwa nguvu na kuipa mafanikio.
Mara baada ya Jaja raia wa Brazil kufunga mabao mawili katika mechi ambayo Yanga iliishinda Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii kwa mabao 3-0, kejeli nyingi zilianza kusukubwa kwa Okwi.
Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimbeza kwa ujumbe wa kila aina wakidai hawamhitaji tena.
Uongozi wa Yanga umeamua kwenda Fifa kuhakikisha Okwi hachezi Simba kwa madai kuwa ni mchezaji wao na inamdai fedha.
Lakini OKwi naye kupitia mwanasheria wake Dk Damas Daniel Ndumbaro nayo imefungua madai kuidai Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment