Unaweza kudhani Louis van Gaal amelala na anasajili washambuliaji tu, la! Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni kufungwa, Manchester United imemnasa beki kisiki wa Ajax, Daley Blind.
Blind anayeweza kucheza kama beki wa kushoto, beki wa kati au kiungo
mkabaji ‘ameikost’ Man United pauni milioni 14.
Mkali huyo ambaye ni mwanasoka bora wa Uholanzi msimu uliopita akiwa na
Ajax, pia alikuwa kwenye kikosi cha Uholanzi kilichoshika nafasi ya tatu kwenye
Kombe la Dunia, kocha akiwa van Gaal.
Ilikuwa inaonekana wazi kwamba Man United ina tatizo kubwa kwenye ulinzi
na sasa kocha huyo atakuwa amelipatia ufumbuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment