September 14, 2014




Yanga imebeba Ngao ya Jamii na kuitungua Azam FC kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Pamoja na kuifunga Azam FC, Yanga imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania Bara kuifunga Azam FC ambayo ilimaliza mechi 26 bila kufungwa hata moja.
Angalau lingekuwa bao moja, lakini ndani ya dakika 45, Yanga imefunga mabao matatu ambayo ukiyagawa unapata bao moja kila baada ya dakika 15.
Azam FC ilicheza vizuri na kutawala kipindi cha kwanza, lakini mambo yakabadilika katika kipindi cha pili.

Mshambuliaji Mbrazil, Jaja ameifungia Yanga bao la pili katika mechi inayoendelea kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar.
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jaja alifunga alifunga mabao yake katika dakika ya 58 kabla ya kupachika la pili katika dakika ya 64.
Simon Mvuva akafunga la tatu katika dakika ya 88 baada ya kipa Mwadini Ally kujichanganya na mfungaji akautupia nyavuni kwa ulaini kabisa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic