Kiungo Maroaune Fellaini ambaye amekuwa
hakubaliki katika kikosi cha Man United, leo amefunga bao safi kabisa na
kuisaidia Man United kuamka katika sare yake ya mabao 2-2 dhidi ya wenyeji wake
Wes Brom.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England, katika
dakika ya 48, Fellaini alifunga bao akiwa ndiyo anagusa mpira wake wa kwanza
baada ya kuingia akitokea benchi katika kipindi cha pili. Kabla ya kufunga
aliweka mpira gambani, akadanganya kabla ya kupiga shuti kali.
Bao hilo lilikuwa la kusawazisha baada ya
Stephane Sessegnon aliyekuja nchini na timu yake ya taifa ya Benin iliyochapwa
na Stars bao 4-0, kuanza kuipatia Wes Brom bao safi. Bao lake alilifunga katika
dakika ya 8 tu.
Fellaini aliendelea kufanya vizuri katika
kiungo hata baada ya Barahino kufunga bao la pili akiwatoka mabeki wa Man
United waliojichanganya katika kuweka mtego wa offside.
Bao hilo la Berahino katika dakika ya 66,
halikuikatisha tamaa Man United iliyoendelea kupambana hadi dakika ya 87
ilipopata bao hilo kupitia Blind aliyepiga mkwaju mkali baada ya Falcao kumpa
pasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment