LIVERPOOL, England
PAMOJA na kuwa katika wakati mgumu akionekana
hafungi licha ya kwamba amenunuliwa kwa kitita cha pauni milioni 16 (Sh bilioni
37) kutoka AC Milan, mshambuliaji Mario Balotelli ndiye anaongoza kwa wastani
mzuri wa mashuti langoni.
Soka lina misemo yake na unapozungumzia wapiga
mashuti basi wenyewe wanawaita wapiga mawe.
Balotelli tayari ana wastani wa mashuti mengi
anayopiga na kulenga lango kuliko mchezaji mwingine wa Ligi Kuu England.
Balotelli ana wastani wa mashuti matano katika
kila mchezo aliocheza ambayo amepiga na kulenga lango.
Hii inaonyesha wakati wowote anaweza kurejea
kwenye listi ya wachezaji wanaofunga kwa kuwa mashuti yake yanalenga lango
zaidi.
Wanaomfuatia ni Graziano Pelle wa Southampton,
Sergio Aguero (Man City) na Diego Costa wa Chelsea ambao kila mmoja ana wastani
wa mashuti manne kwa mechi.
Hapa kuna kitu kinaonyesha kuwa Balotelli yuko
kwenye kundi la washambuliaji hatari kwa maana ya kupiga mashuti, lakini
ameshindwa kuwa mjuzi zaidi na kufunga.
Washambuliaji wenye wastani wa mashuti manne
kila mmoja ambao wako chini yake kiwastani kwa mashuti, ndiyo wanaosumbua kwa
ufungaji mabao.
Costa ndiye anaongoza ufungaji bora akiwa na
mabao kumi (kabla ya mechi ya jana), Aguero ana matano na Pelle amepachika
manne.
Hivyo ni kazi kwake kurekebisha mambo na
kufanya aingie kwenye listi ya wapachika mabao na si wapiga mashuti yanayolenga
tu.
Kwa upande wa timu, Chelsea wamefunga mabao 19
kabla ya mechi ya jana dhidi ya Arsenal wakifuatiwa na Man City wenye 14.
Wao pia ndiyo wanaongoza kwa wastani wa kupiga
mashuti mengi yaliyolenga lango wakiwa na 18 kwa mechi moja.
Man City wanawakimbiza kwa karibu wakiwa na
wastani wa mashuti 17 kwa mechi moja, halafu Liverpool wenye 16 na Arsenal wana
15.
Hii ni mapema sana kwenye ligi hiyo, lakini
kila baada ya mechi moja au mbili kunakuwa na mabadiliko kwa kuwa wachezaji
wanang’amua kipya cha kufanya, hali kadhalika makocha.
Mashuti kwa mechi:
Chelsea 18
Man City 17
Liverpool 16
Arsenal 15
Newcastle 14
Mashuti kwa mechi:
Mario Balotelli - Liverpool 5
Graziano Pellè - Southampton 4
Sergio Agüero-Man City 4
Diego Costa -Chelsea 4
Charie Austin-QPR 3
0 COMMENTS:
Post a Comment