BASENA (CHINI KULIA) AKISHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA. KUSHOTO KWAKE NI MWINA KADUGUDA NA MINHAL DEWJI, MTOTO WA KATIBU MKUU WA ZAMANI WA SIMBA, KASSIM DEWJI. |
Aliyekuwa bosi wa benchi la ufundi la Simba, Moses Basena amerejea jijini Dar es Salaam, kimyakimya.
Basena alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wakati kocha akiwa Zdravko Logarusic.
Hata hivyo, aliondolewa baada ya Simba kuamua kutokuwa na nafasi hiyo.
Lakini jana alionekana akiwa kwenye Uwanja wa Taifa upande wa VIP akifuatilia kwa umakini mkubwa mechi ya watani Yanga na Simba.
Bado hakuna taarifa za uhakika aliamua kurejea kushuhudia mechi hiyo au ana mpango wa kurejea Msimbazi.
Basena pia aliwahi kuwa kocha mkuu wa Simba, wakati huo Yanga ikinolewa na Sam Timbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment