Si unajua wachezaji
wanapenda kushangilia kwa sarakasi kama ilivyokuwa kwa Luis Nani aliyekuwa Man
United, sasa yuko Sporting Lisbon ya Ureno. Sasa watambue hiyo ni hatari.
Mchezaji mmoja wa India
amefariki dunia wakati akijaribu kushangilia baada ya kufunga bao kwenye Ligi
Kuu Soka nchini India.
Peter Biaksangzuala amefariki
dunia jana Jumapili wakati akitibiwa hospitalini.
Mara baada ya kuifungia
timu yake ya Bethlehem Vengthlang FC alikimbia kwenda kushangilia na kujaribu
kuruka ‘samasoti’, akaanguka vibaya na kuvunja uti wa mgongo.
Kijana huyo aliyekuwa na
umri wa miaka 23 alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 62 dhidi ya Chanmari
West FC.
Kocha wa zamani wa Man
United, Alex Ferguson aliwahi kumzuia Luis Nani kuruka sarakasi wakati wa
kushangilia bao.
0 COMMENTS:
Post a Comment