Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba
iliyochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza
sh. 427,271,000.
Washabiki
49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh.
7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya
tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.
Kwa
upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa
kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh.
24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh.
10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh.
71,341,186.86.
0 COMMENTS:
Post a Comment