Kocha Patrick Phiri amesema daktari wa Simba amemhakikishia kiungo Jonas Mkude atarejea dimbani ndani ya siku tano.
Phiri raia wa Zambia amesema Mkude aliyeteguka bega, anaendelea vizuri.
"Nimefurahi kusikia atarejea haraka, Wanasimba wasiwe na wasi kuhusiana na kijana wao.
"Wakati anatolewa uwanjani, kidogo alituogopesha maana alikuwa akilia, kilikuwa si kitu kizuri.
"Lakini kama atapona mapema, ni jambo zuri kwetu sote," alisema Phiri.
Mkude aliumia katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo ilimalizika kwa suluhu.
0 COMMENTS:
Post a Comment