Mshambuliaji nyota wa Hispania, Diego Costa ameingia kwenye lawama kama zile ambazo hupata washambuliaji wengi wa Afrika kuwa wanajituma kwenye klabu zao lakini hawafanyi vizuri na timu za taifa.
COsta anaongoza kwa upachikaji mabao England akiwa na tisa, lakini inaonekana hana msaada na Hispania.
Hiyo inatokea baada ya Hispania kulambwa kwa mabao 2-1 na Slovakia ambayo haina mastaa wengi.
Vyombo vya habari vya Hispania, vimekuwa vikimuandama tokea jana na kutoa takwimu zinazoonyesha alicheza katika kiwango cha chini katika mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment