Mshambuliaji Luis Suarez
alilazimika kutoka kasi uwanjani na kukimbilia msalani wakati mechi ikiendelea, lakini kwa ruhusa ya mwamuzi.
Suarez alifanya hivyo
wakati Uruguay ikiwa ugenini inaivaa Saudi Arabia katika mechi ya kirafiki.
Yeye ndiye alikuwa shujaa
kupiga krosi safi ambayo ilisababisha bao la kuongoza baada ya beki wa Saudi
Arabia kujifunga, lakini wenyeji wakasawazisha baadaye.
Suarez bado anatumikia
adhabu ya miezi minne kutocheza baada ya kumuuma Girgio Chiellini wa wakati wa
Kombe la Dunia.
Lakini ameruhusiwa
kucheza mechi ambazo si za mashindano za kimataifa kama hiyo dhidi ya Saudi
Arabia.
0 COMMENTS:
Post a Comment